Mtu mmoja aliejualikana kwa jina la Focus Juma mkazi wa kijiji cha Nkiniziwa wilaya ya Nzega mkoani Tabora amekamatwa kwa tuhuma za kukata umeme kwa shoka na kuacha nyaya zikining'inia huku akiacha baadhi ya vijiji kukosa umeme.
Kwa mujibu wa taarifa za shirika la umeme (TANESCO) mtuhumiwa wakati akitekeleza tukio hilo la kukata nguzo inayosafirisha umeme mkubwa wa Kilovolt 132 alipigwa shoti na kunusurika kifo.
Baada ya tukio hilo mtuhumiwa alikimbizwa katika kituo cha afya Busondo wilayani Nzega akiwa hajitambui huku akiwa ameungua sehemu mbalimbali za mwili ikiwemo miguuni,shingoni na mikononi.
TANESCO Mkoani Tabora bado wanaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu chanzo cha mtuhumiwa huyo kufanya kitendo hicho.
0 Maoni