Wakala wa Usajili Biashara na Leseni (BRELA) imesema leseni ya kampuni iitwayo Kalynda E-Commerce ilitolewa Juni 21, 2022 ni kwaajili ya uuzaji wa jumla wa vifaa vya kieletroniki na mawasiliano pamoja na ufanyaji wa biashara ya kiteknolojia ya kimataifa mtandaoni.
BRELA imesema kumekuwa na taarifa zinazoleta taharuki kuhusu kampuni hiyo kufanya biashara ya upatu ya kukusanya fedha kutoka kwa wananchi kwa ahadi ya kupata faida ndani ya muda fulani kinyume na bidhaa au huduma iliyoombewa leseni.
Aidhaa BRELA imetoa angalizo kwa umma kuwa kabla ya kuingia kwenye mahusiano ya kibiashara na kampuni yoyote ni vema kupata uthibitisho wa uhalali na uwepo wa kampuni hiyo pamoja na biashara husika kutoka BRELA na mamlaka nyingine za serikali.
0 Maoni