TANGAZA HAPA

Mzee wa miaka 64 mbaroni kwa kubaka mwanafunzi

ABOUBAKAR Said (64), mkazi wa Kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga, anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kidato cha kwanza baada ya kumrubuni kwa kumpa shilingi elfu 10.

Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo Jackson Mwakagonda, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema mtuhumiwa huyo alifanya kitendo hicho cha ukatili Oktoba 10, 2022 majira ya saa 8:00 mchana.

Amesema baada ya tukio hilo mtuhumiwa amekamatwa na uchunguzi utakapokamilika atafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria.

Aidha, Kaimu Kamanda huyo amewataka wazazi na walezi kuimariha ulinzi kwa watoto wao ili kuwaepusha na vitendo vya ukatili.

Chapisha Maoni

0 Maoni