mwanafunzi wa shule ya msingi Chalinze Modern Islamic, Iptisum Slim
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limesema linafanyia kazi tuhuma alizozitoa mwanafunzi wa shule ya msingi Chalinze Modern Islamic, Mkoa wa Pwani, Iptisum Slim aliyedai kubadilishiwa namba yake ya mtihani wa kumaliza elimu ya msingi Oktoba 5-6, 2022.
Kupitia video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii mwanafunzi huyo mhitimu wa darasa la saba, 2022 amemuomba Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda kuingilia kati madai ya kufanya mtihani na namba ambayo si yake.
Leo Oktoba 14 kupitia taarifa iliyotolewa na Afisa Habari na Uhusiano Necta, John Nchimbi imeeleza baraza hilo linafanyia kazi taarifa hiyo ili mwanafunzi huyo apate haki yake.
0 Maoni