Rais Samia Suluhu Hassan ameziagiza Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) na Mamlaka ya kuzuia rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) kufuatilia miradi ya maendeleo iliyobainika kuwa na dosari.
Aidhaa Rais Samia amezitaka TAKUKURU na ZAECA kuwachukulia hatua wasimamizi wa miradi iliyobainika kuwa na ufujaji,wizi,matumizi mabaya ya fedha pamoja na rushwa.
Vilevile Rais Samia amewataka viongozi na watendaji wahakikishe wanasimamia matumizi sahihi ya fedha zinazoelekezwa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
0 Maoni