TANGAZA HAPA

miaka 30 jela kwa kubaka mtoto 16

Mkazi wa Kata ya Magugu Wilayani Babati mkoani Manyara, Shabani Jumanne amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kumbaka binti wa miaka 16.

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Babati, Victor Kimario jana Alhamisi Oktoba 13, 2022.

Hakimu Kimario ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo amekutwa akifanya tukio hilo Julai 28, 2022 katika choo cha nyumbani kwa msichana huyo ambaye ni mlemavu wa kusikia na kuongea.


CHANZO: Mwananchi

Chapisha Maoni

0 Maoni